BurundiIndundi CinemaMoviesswahili

Breaking News : Kifo cha baba yake mzazi Lolilo /Mumivu makali kwa Lolilo

Nyota wa Music wa Buja Flever pia na muigizaji wa Filamu nchini Burundi Lolilo kupatwa na kilio na kuondokewa na Baba yake Mzazi, hapo ni baada ya siku chache baba yake mdogo kuaga dunia ambae ni mdogo wa baba yake Lolilo ,kwasasa kilio kimeanguka pia kwa mkubwa. Tulipo wasiliana na Lolilo amesema :

Kusema Ukweli nina masikitiko makubwa sana kuondokewa na Baba yangu, kweli alikuwa mgonjwa sana ila imani yangu imekuwa kwamba najuwa tu lazima atapona ila baada ya Baba mdogo kufariki kweli hali Ya baba yangu imezidi Kuwa mbaya hadi leo umauti unamkumba, kweli inauma ila sina jinsi maana mipango ya Mungu haina makosa ,ila naomba tu Mungu atujalie mwisho mwema na amlaze baba yangu mahali pema peponi”.

Lolilo ni MSANII mkubwa sana nchini Burundi lea upande wa muziki pia na Filamu ,Msiba huu ni pigo kwa  wasanii wenzake.

What's your reaction?

Related Posts

1 of 149