africa newshomepageMoviesNigeriaswahili

#Nigerian Film: Genevieve Nnaji amepewa rasmi heshima ya kuwa memba wa Academy of Motion Picture Arts and Science

Genevieve Nnaji amepewa rasmi heshima ya kuwa member wa Academy of Motion Picture Arts and Science na hivyo kuanzia sasa ataweza kupiga kura kuchagua washindi wa tunzo za Oscars ambazo ndio tuzo kubwa zaidi za filamu duniani.

Genevieve amepata mwaliko huo ambapo ataweza kuwa na nguvu ya kumpigia kura washindi kwa miaka 10 ijayo, pamoja na kuwa akitumia vizuri nafasi ataweza kupata fursa nyingi za yeye binafsi. Akin Omotoso director wa Nigeria pia amepata heshima hiyo hivyo kuungana na kina Omotola Jalade

Mastaa wengine walioalikwa mwaka huu ni pamoja na Zendaya, Eva Longoria na kwa Bollywood ni Hrithik Roshan na Alia Bhatt ambao Genevieve ataweza kukutana nao, pamoja na directors, producers, distributors wakubwa marekani, ulaya, asia pamoja na technicians wenye ujuzi mkubwa.

Academy wamemtambua Genevieve Nnaji kupitia filamu zake za Road to Yesterday na Lionheart ambayo licha ya kuwa filamu ya kwanza Nigeria kutumwa tunzo za Oscars 2019 lakini ilitupwa nje bila hata kupita hatua za mchujo wa awali sababu ya dioloji kubwa kuwa ya kiingereza badala ya lugha ya kinaigeria au isiyo English. Mwaka huu wamealikwa 819 toka nchi mbalimbali hasa Ulaya, Asia na Marekani, wakikubali wote waliolikwa mwaka huu jumla ya jopo la Oscars litakuwa 9412 katika kuchagua washindi

Ikiwa kwamba waigizaji wa Burundi watajituma lazima wafikie Malengo yao.

What's your reaction?

Related Posts

1 of 247